WAKATI homa za wasanii mbalimbali juu ya shindano la Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) zikizidi kupanda, wadhamini wa shindano hilo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, imeandaa kipindi cha runinga kitakachozungumzia juu ya tuzo hizo. Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Meneja wa bia ya Kilimanajro Premium Lager, Pamela Kikuli, na kueleza kuwa kipindi hichi kitaitwa ‘Kili Chats.’ Alisema sio mara ya kwanza kwa bia hiyo kuandaa kipindi cha aina hii kwani mwaka jana kilirushwa wakati wa msimu wa ‘Nani Mtani Jembe’, kampeni inayowashirikisha wakongwe wa soka hapa nchini Simba na Yanga. Meneja huyo alisema sasa hivi wameamua kujikita katika muziki kwani ndio msimu wa KTMA kwa hivyo wanataka kusikia kutoka kwa wananchi kuhusu maoni yao. “Huu ni mwanzo mzuri kuelekea KTMA ambapo tutaalika wadau mbalimbali kwa mfano Ma DJ, wanamitindo, washiriki katika video mbalimbali na wengine,” alisema Pamela. Alisema kipi...
HII NI BLOG KWA AJILI YA KUPASHANA HABARI MBALIMBALI ZA KISIASA, MICHEZO NA BURUDANI, HABARI ZINAZO JITOKEZA KATIKA JAMII ZETU.