WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ametangaza rasmi kuwania urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM}, huku akitamba ataipeleka nchi katika uchumi wa viwanda unaobebwa na kilimo na kuahidi kujenga serikali ya waadilifu. Licha ya Membe, wana CCM wengine wawili jana walitangaza pia kugombea urais nao ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Januari Makamba pamoja na Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangala. Membe alifichua kuwa alienda kuomba kwenye kaburi la Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ili kupata ridhaa na kusisitiza kuwa urais si suala la kukurupuka na kwamba atahakikisha anasimamia utawala bora, huku akiongoza mapambano dhidi ya rushwa na kwa kubadili kipengele cha mtu atakayetoa rushwa na kutoa taarifa awe huru. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya CCM Mkoa wa Lindi jana, Waziri Membe alisema kabla ya kuchukua uamuzi wa kufikiria urais alijipima na kuona anatosha kwa nafasi hiyo, pia baada ya kuwaangali...
HII NI BLOG KWA AJILI YA KUPASHANA HABARI MBALIMBALI ZA KISIASA, MICHEZO NA BURUDANI, HABARI ZINAZO JITOKEZA KATIKA JAMII ZETU.